Mkurugenzi Mkuu wa shirika la umeme Tanzania – TANESCO, Maharage Chande amesema watahakikisha wanaongeza nguvu kwenye usimamizi wakati wa kumalizia asilimia 15 za Ujenzi wa mradi wa Bwawa la kufua umeme JNHPP, zilizobaki ilimnchi iwe na umeme wa uhakika.
Chande ameyasema hayo hii leo Aprili 25, 2023 wqkati wa ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Bwawa hilo linalojengwa Mto rufiji Mkoani Pwani akiambatana na Waziri wa Nishati, Januari Makamba.
Amesema, “usimamizi ni muhimu ili kufanikisha lengo na tutahakikosha tunaongeza nguvu katika eneo hili muhimu maana kukamilika kwake kutawezesha ufikiaji wa malengo ya kiuchumi na kuwa na umeme wa uhakika.”
Kukamilika Kwa mradi huo wa kuzalisha umeme megawati 2115, kutawezesha kusisimua uchumi wa Tanzania kwani kutakuwa na uhakika wa Nishati hiyo itakayotumika maeneo mbalimbali muhimu ikiwemo viwandani na kwenye migodi.