Uongozi wa Wakala wa Taifa wa Uzalishaji na Uendelezaji wa mbegu za kilimo – ASA, umetakiwa kuendelea kuzingatia ubora na weledi katika majukumu yao ya kuzalisha mbegu bora, ili kuendelea kuwa na uhakika wa chakula cha kutosha nchini.

Wito huo, umetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga wakati wa ziara yake ya kufuatilia shughuli za utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo na Uvuvi – AFDP, Mkoani Morogoro, inayoratibiwa na ofisi yake na kutekelezwa katika mikoa mbalimbali nchini.

Amesema, upo umuhimu wa kuendelea kuunga mkono Programu ya kuendeleza Sekta ya Kilimo na Uvuvi, kwani inaongeza tija hasa katika kuhakikisha kunakuwa na mbegu bora nchini, huku akiwataka kuzingatia uzalishaji wa mbegu bora zinazoendana na mahitaji halisi.

Akiwa katika ziara hiyo, Nderiananga alitembelea Kituo cha Kuendeleza Ukuzaji Viumbe Maji Kingolwira, Wakala wa Taifa wa Uzalishaji na Uendelezaji wa mbegu za kilimo – ASA, na Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania – TOSCI, zilizopo Mkoani Morogoro.

Wizara, Wadau wapanga mikakati kudhibiti matukio ya ujangili
Mkuu wa Mkoa wa zamani ashitakiwa kwa mauaji