Waziri wa Nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Ummy Mwalimu ameelekeza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuwasilisha Maombi ya fedha nakuhakikisha mkandarasi anapatikana kabla ya Novemba 15.
Asema kufikia Novemba 15 maombi ya fedha na mkandarasi yawe yamekamilika.
Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan*ametoa kiasi Cha Shilingi bilioni 32.2 kwaajili ya Ujenzi wa Soko jipya la Kariakoo na kukarabati Soko lililoungua kwa Moto.
Waziri Ummy amesema Katika mchanganuo wa matumizi ya Kiasi hicho Cha bilioni 32.2, kiasi Cha Shilingi bilioni 6 zitakarabati Soko lililoungua na Shilingi bilioni 26.2 zitakwenda kujenga Soko jipya la Gorofa 6 kwenda juu na Gorofa 2 kusuka Chini.
Akizungumza wakati wa ziara ya kutekeleza maelekezo ya Rais Samia kuhusu maboresho Soko la Kariakoo akiambatana na Naibu waziri wa Fedha Mhe. Hamad Masauni, Waziri Ummy amesema Soko hilo jipya litakuwa na uwezo wa kuchukuwa zaidi ya Wafanyabiashara 2,000 tofauti na Sasa ambapo Lina uwezo wa kuchukuwa Wafanyabiashara 600 pekee.
Pamoja na hayo amewataka Wafanyabiashara wa Soko dogo kuwa tayari kuondoka ili kupisha Ujenzi wa Soko Hilo jipya na kusema Ujenzi utakapomalizika kipaombele kitatolewa kwa walewale wa awali.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa Mstari wa mbele kushughulikia changamoto za Wafanyabiashara.
Aidha RC Makalla amesema *kabla ya kuwahamisha Wafanyabiashara wa Soko dogo, Serikali itahakikisha inachukuwa taarifa zote za Wafanyabiashara hao ili Ujenzi ukimalizika kipaombele Cha kwanza kiwe Ni kurejeshewa maeneo yao ya Biashara.