Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, amezitaka shule zote msingi na sekondari nchini kuanzia Septemba Mosi kuweka mazingira wezeshi kwa wanafunzi kunywa maziwa shuleni kwa kufungua migahawa ya maziwa

Waziri Mwalimu ameyasema hayo leo Ijuma katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma, wakati wa ufunguzi wa siku ya lishe kitaifa pamoja na kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani.

Amesema kuwa shule ziwape wajasiriamali kuuza nafasi ya kufungua vibanda vya kuuzia maziwa, huku akivitaka viwanda kuwa na uwezo wa kutengeneza maziwa yenye ujazo angalau ujazo wa Mils 100, ili kukidhi mahitaji ya gharama na ununuzi kwa kila mtoto.

“Nitamuandikia Waziri Ndalichako, maana yeye ndio anasimamia shule zote za serikali na binafsi” Amesema.

Lebanon: waandamana kutaka viongozi wajiuzulu
Makatibu wa SADC wakutana kuboresha rasimu za nyaraka na kimkakati

Comments

comments