Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kuwa wananchi hawapaswi kununua damu kwani huduma hiyo ni bure kwa watanzania wote katika hospitali zote.

Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait katika Taasisi ya Mifupa MOI ambapo ulihudhuliwa na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania.

“Watanzania wanahoitaji huduma ya kuongezewa damu wapewe bure marufuku kwa watoa huduma za vituo vya afya pamoja na hospitali zote kuuza damu hiyo kwani inatoka kwa wananchi wenyewe,” amesema Ummy.

Amesema kuwa wananchi wanatakiwa kujitokeza katika kuchangia damu ili kuweza kuwa na hifadhi ya kutosha na kufanya kazi kwa wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo kwa wakati sahihi bila ya usumbufu wowote katika kuokoa maisha ya watanzania.

Kwa upande wake Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania, Jasem Ibrahim Al-Najem amesema kuwa  wameamua kuchangia kiasi cha fedha cha shilingi Milioni 200 katika kutengeneza Benki hiyo ya damu MOI ili kuweza kusaidia kuboresha sekta ya afya nchini.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Lwezimula amesema kuwa katika kuhakikisha Matibabu ya kibingwa yanapiga hatua nchini waliamu kuanzisha kambi za matibabu kuanzia mwaka 2000 na kufanya taasisi zingine za afya kuiga mfano huo.

 

Magazeti ya Tanzania leo Novemba 4, 2017
Ligi ya wanawake 2017/18 kuanza mwezi huu