Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amempongeza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa jitihada zake za kupambana na masuala ya UKIMWI nchini.

Ummy ameyasema hayo katika Kilele cha Mdahalo wa Kitaifa Juu ya Kuimarisha Ubia Baina ya Serikali, Wadau na Jamii kwa Uendelevu wa Mafanikio ya Mwitikio wa UKIMWI nchini, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, Dodoma.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akiteta jambo na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Bungeni jijini Dodoma.

Amesema, “Mheshimiwa Waziri Mkuu kutokana na juhudi zako, maelekezo na uamuzi wa kuwa Balozi wa kuhamasisha Wanaume kupima maambukizi ya VVU.”

Aidha, Waziri Ummy pia amebainisha kuwa uelewa kwa Watanzania wanaofahamu hali zao kuhusu VVU umeongezeka kutoka asilimia 61 mwaka 2016/2017 hadi kufikia asilimia 97 mwaka 2023.

Miquissone, Kramo wamchanganya Robertinho
Tanzania yavuka lengo mapambano dhidhi ya VVU