Baraza la usalama la umoja wa mataifa linatarajiwa kuanza kuweka vikwazo vipya dhidi ya Korea Kaskazini katika kupinga jaribio la silaha za kinyuklia lililofanywa na Pyongyang.

Korea kusini imesema itahakikisha inainalishawishi baraza hilo kuweka vikwazo dhabiti ili kuizuia Korea Kaskazini kuendelea na mpango wake huo wa majaribio ya silaha za nyuklia katika ukanda huo kwani ni hatari zaidi.

Serikali ya Marekani na korea kusini zimeungana kufanya uchunguzi wa hewa na bahari kuchunguza athari ya vifaa vya mionzi vilivyotumika katika jaribio hilo, ili ziweze  kubaini ni silaha gani iliyofanyiwa majaribio.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilikutana na kutoa taarifa ya kuikosoa vikali majaribio hayo ya Korea Kaskazini.

Rusia na Marekani Kumaliza Vita Nchini Syria
Mchungaji Rwakatale Atenga Milioni 25 Kwaajili Ya Kuwarejesha Wafungwa Uraiani