Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wametoa wito wa kufanyika kwa mazungumzo ya kumaliza ghasia zinazozidi kumwaga damu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). 

Ujumbe wa mabalozi uliotumwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ulikutana na Rais Félix Tshisekedi mjini Kinshasa, na ulikwenda Goma siku ya Jumamosi ambapo ulikutana na viongozi wa eneo hilo na kutembelea kambi ya wakimbizi wa ndani.

Mjumbe wa ujumbe huu, balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa, Nicolas de Rivière, amewaambia waandishi wa habari kwamba M23 wanapaswa kujiondoa katika maeneo wanayoyashikilia, na kuongeza kuwa hakuna tena haja ya kuonyesha kwamba Rwanda inaunga mkono M23 na kwamba wanajeshi wa Rwanda mara kwa mara hufanya uvamizi katika mkoa wa Kongo wa Kivu Kaskazini, ambao Goma ni mji mkuu wake.

Nicolas de Rivière, Balozi wa Ufaransa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na mwenzake wa Gabon Michel Xavier Obiang, wanawasili katika makao makuu ya MONUSCO huko Goma mnamo Picha: AFP – GUERCHOM NDEBO

“Njia ya kutoka kwa mzozo huu inaweza tu kuwa ya kisiasa, na inaweza kupatikana tu kupitia mazungumzo,” amesisitiza.

Mjumbe mwingine, balozi wa Gabon katika Umoja wa Mataifa Michel Xavier Biang, amekiri, akisema kwamba diplomasia lazima itawale.

Ziara hii inajiri mara tu baada ya kushindwa kwa usitishaji mapigano mashariki mwa DRC, uliojadiliwa na upatanishi wa Angola na kuvunjika siku ya Jumanne, siku hiyo ulipoanza kutekelezwa.

Mipango mingine kama hiyo ya amani imeshindwa huko nyuma. Eneo la Mashariki mwa DRC, linalopakana na Rwanda limekuwa likikumbwa na kuzuka kwa ghasia tangu waasi wa M23 walipochukua silaha tena mwishoni mwa 2021, na kuteka maeneo yote ya eneo hilo.

Wapiganaji wa M23 pia walisonga mbele katika siku za hivi karibuni, wakitishia kufunga barabara zote za kuingia Goma, jiji kuu la mashariki mwa DRC, karibu sana na Rwanda na ambalo lina zaidi ya wakazi milioni moja.

Mapigano kati ya majeshi ya Kongo na M23, ambayo DRC na mataifa mengine yanasema yanaungwa mkono na Rwanda, hadi sasa yamesababisha zaidi ya watu 800,000 kuyatoroka makaazi yao, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Siku ya Jumamosi, raia watano waliuawa kwa mashambulizi ya angani wakati wa mapigano kati ya vikosi vya Kongo na waasi wa M23 huko Kahumiro, kilomita 120 kaskazini mwa mji wa Goma, kulingana na maafisa wa usalama na wakaazi.

Lakini pia wataalam wa Umoja wa Mataifa, Marekani, Ufaransa na nchi nyingine kadhaa wanabaini kwamba Rwanda inaunga mkono moja kwa moja M23, madai ambayo Kigali inakanusha.

TLP yapewa siku sita na msajili wa vyama vya siasa
Achanganyikiwa kwa kugombaniwa na Warembo