Umoja wa nchi 28 Barani Ulaya zimekutana kwa ajili ya kusaka msimamo wa pamoja kuhusu kushambuliwa kwa Syria huku baadhi ya nchi zikihofia msimamo utakaochukuliwa na Urusi ambayo ndiye msambazaji mkuu wa gesi barani humo.
Umoja huo wa Ulaya unataka kujaribu kuangalia jinsi ya kushughulikia mgogoro wa kidiplomasia ulioibuka na Urusi kufuatia suala la kushambuliwa kwa Syria.
Aidha, Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Umoja wa Ulaya wanataka kuwa na msimamo wa pamoja na hatimaye kuwa na mshikamano kufuatia mgawanyiko uliojitokeza baada ya mashambulizi yaliyofanywa nchini Syria.
Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Ulaya wamepinga vikali kuchukuliwa kwa hatua ya aina yeyote ambayo inaweza kusababisha mgogoro huo kuongezeka.
Hata hivyo, Mkutano wa leo unatarajia kujadili jinsi ya kuishinikiza Urusi kujaribu kuumaliza mgogoro wa Syria, ingawa hadi sasa nchi kadhaa za Umoja wa Ulaya zimeshindwa kuzungumzia hatua ya kushambuliwa kwa Syria kwa sababu ya wasiwasi kuhusu msimamo utakaotoka Urusi ambayo ni miongoni mwa nchi muhimu inayosambaza gesi barani Ulaya.
-
Comey amponda Trump, adai hana sifa ya kuwa rais
-
Iran yadai mashambulizi ya Marekani hayana athari zozote
-
Trump apigilia msumari Syria, ajipanga kuipiga tena