Wakuu wa Nchi za Umoja wa Ulaya na Nchi 3 za Afrika wamekubaliana kuhusu mpango wa kupunguza idadi ya wahamiaji wanaoelekea Ulaya, na pia kukabiliana na uhamiaji haramu.
Mataifa manne yenye nguvu za ushawishi mkubwa barani Ulaya pamoja na nchi tatu za Afrika zimekubaliana kuwe na mpango wa kukabiliana na usafirishaji haramu wa binadamu.
Aidha, kwa muda mrefu, Umoja wa Ulaya unaoundwa na nchi wanachama 28 umekuwa ukitafuta njia mbadala ya kuweza kukabiliana na wimbi kubwa la wahamiaji haramu ambalo limekuwa likimiminika barani humo.
Mwenyeji wa mkutano huo uliowakutanisha wakuu wa nchi za Ujerumani, Italia, Uhispania, Chad, Niger na Libya kujadili suala hilo, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema kuwa wakati umewadia wa kuwa na mpangilio imara
Viongozi hao wamekubaliana kuwa na mpango wa pamoja wa kuanza kuwatambua wahamiaji halali wanaokimbia vita au waliopo katika kitisho cha kuuawa na kutumia Umoja wa Mataifa kuwasajili nchini Niger na Chad kama hatua ya kuwazuia dhidi ya unyanyasaji kutoka kwa wasafirishaji haramu wa binadamu.
-
Watuhumiwa wa kula nyama za binadamu wakosa dhamana
-
Korea Kaskazini yaianzishia chokochoko Japan
-
Israel yaituhumu Iran, yaitaka iache mchezo mchafu
Hata hivyo, kumekuwepo na wimbi kubwa la wahamiaji haramu kutoka Mashariki ya Kati, Asia na Afrika ambao wamekuwa wakikimbilia barani humo kwa lengo kukimbia, vita, umaskini na misukosuko ya kisiasa.