Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Wakimbizi Duniani (UNHCR) limejitolea kusimamia mdahalo utakaofanywa kati ya Rwanda na Burundi kuhusu raia ambao ni wakimbizi.
UN imesema hayo pindi ilipomtembelea Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza ambapo walifanya mazungumzo kuhusiana na majanga mbalimbali yanayowakuta wakimbizi.
UN imesema itaendelea kutoa msaada kwa wakimbizi wa Burundi ambao kwa hiari yao wanataka kurudi nchini kwao.
”Tutafanya kazi kutengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya mdahalo kati ya Rwanda na Burundi. Nimeongea na Rais wa Rwanda Paul Kagame na nawahakikishia kuwa yatakuwa ni majadiliano mazuri” Amesema afisa wa UN.
Wiki iliyopita Burundi iliwashutumu Kigali, Rwanda kwa kuwashikilia wakimbizi ambao ni raia wa nchi yao na kudai kuwa Rwanda inawafundisha zaidi ya wakimbizi 2000 wa Burundi mbinu za kivita ili kupindua serikali ya Rais Nkurunziza.