Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linatarajia kupiga kura kuhusu mswada tete utakaozishinikiza Morocco na Polisario kurudi katika meza ya mazungumzo chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa.

Mswada huo ulioandaliwa na Marekani unalengo la kuweka msingi wa mazungumzo ya kusuluhisha mzozo wa Sahara Magharibi uliodumu kwa miongo mingi.

Aidha, mswada unalenga kuishinikiza Morocco na chama cha Polisario kinachoungwa mkono na Algeria, kurudi katika meza ya mazungumzo chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa.

Hata hivyo, Morocco na Polisario zilipigania udhibiti wa Sahara Magharibi kuanzia mwaka 1975 hadi 1991 pale mkataba wa usitishaji mapigano ulipoafikiwa na ujumbe wa na kikosi cha Umoja wa Mataifa uliokuwa unajulikana kama MINURSO.

 

 

 

JPM kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Iringa
Mwakyembe ataja maudhui mtandaoni ni chazo cha mmomonyoko wa maadili Tanzania