Idadi ya watu Duniani, inakadiriwa kufikia watu bilioni 8 huku sehemu kubwa ya ongezeko la watu likishuhudiwa kwenye mataifa yanayoendelea hasa katika bara la Afrika.
Siku ya Jumanne, Novemba 16, 2022 ilichaguliwa na Umoja wa Mataifa kama tarehe ya ishara ya kufikiwa kwa idadi hiyo ya watu bilioni 8 ulimwenguni, ambayo makadirio yake yanatokana na takwimu za kisayansi.
Tanzania, Ethiopia, Nigeria na Congo ni miongoni mwa mataifa 8 ambayo Umoja wa Mataifa unasema yatakuwa nyumbani kwa nusu ya ongezeko la idadi ya watu wengi ulimwenguni, kati ya mwaka 2022 hadi 2050.
Nchini nyingine zitakazochangia ongezeko la watu ulimwenguni, ni pamoja na Misiri, Pakistan, Ufilipino na India huku watunga sera wa kimataifa wakiwa na idadi ya watu itaongeza mzigo kwa serikali nyingi duniani ikiwa ni pamoja na barani Afrika ambako huduma muhimu za jamii bado hazipatikani.