Maafisa kadha wa Sudani Kusini wametumiwa kuhusika katika vitend vya ukatili waliofanyiwa raia wa nchi hiyo na kusababisha kuuliwa karibu watu laki nne na mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi kati ya mwaka 2012 na 2018 wakati ikulipotiwa saini makubaliano ya amani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na wataalamu hao wa kujitegemea wa Umoja wa Mataifa iliyotolewa jana imeeleza kuwa maafisa wa jeshi na serikali wa Sudan Kusini bado wako madarakani licha ya kuhusika katika jinai hizo tajwa dhidi ya raia.
Nchi hiyo ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenye kati ya mahasimu wakuu Riek Machar na Salva Kiir na kupelekea kuingia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe
Mahasimu, Salva Kiir, na Riek Machar
Joseph Monytuil Gavana wa jimbo la kaskazini huko Sudan Kusini na Luteni Jenerali Thoi Chany Reat wa vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo wamebainika kuhusishwa na mauaji makubwa, ubakaji na utumwa wa ngono dhidi ya raia wa nchi hiyo.
Kwa upande wa mamlaka ya uongozi huko Juba imeituhumu Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuwa inaingilia masuala ya ndani ya Sudan Kusini na kupinga matokeo hayo ya uchunguzi wa jopo la wataalamu watatu wa Umoja wa Mataifa.