Umoja wa Mataifa umeingilia kati sakata la Bobi Wine na kutaka uchunguzi huru ufanyike juu ya kukamatwa na kuteswa kwa wabunge kadhaa, akiwemo nyota huyo wa zamani wa muziki.

Mkuu wa Kamisheni ya Haki za Binaadamu ya Umoja wa Mataifa, Zeid Ra’ad Al Hussein, ametoa wito kwa serikali ya Rais Yoweri Museveni kuhakikisha unafanyika uchunguzi huru juu ya ghasia hizo, yakiwemo madai ya mauaji ya makusudi, matumizi ya nguvu kupita kiasi na mateso yaliyofanywa na polisi.

“Nimekuwa na wasiwasi hasa kuhusu tuhuma kwamba vikosi vya usalama vimewatesa na kuwatendea vibaya mahabusu. tumepokea pia taarifa za namna mauaji yalivyofanyika na ukamatwaji ovyo ovyo dhidi ya raia wakati wa maandamano.”amesema Zeid

Aidha, dereva wa mbunge Kyagulanyi alipigwa risasi na kuuawa akimsubiri bosi wake kwenye maegesho ya magari mjini Arua, huku polisi ikimkamata mbunge huyo na wenzie watatu, mbunge mmoja mstaafu na mbunge mwengine mteule waliokuwa kwenye chumba cha hoteli.

Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa za Ofisi ya Haki za Binaadamu ya Umoja wa Mataifa, watu wengine 28 walikamatwa, wakiwemo waandishi wawili wa habari na wanawake wawili.

 

 

Video: Lowassa ashtuka, Tamko la Serikali mwanafunzi aliyeuawa Bukoba
Habari kubwa katika magazeti ya leo Agosti 30, 2018