Umoja wa Mataifa (UN) imepitisha kwa kura zilizopigwa na wajumbe kuondoa bangi katika orodha ya dawa za kulevya hatari, hatua ambayo inaonesha huenda ni kuanza kutambua mmea huo kuwa na chembe za tiba.

Wajumbe 27 walipiga kura za ndio kuunga mkono huku wajumbe 25 wakipiga kura za hapana. Nchi zilizopiga kura kuunga mkono ni pamoja na Marekani, Uingereza, Ujerumani na Afrika Kusini.

Pakistan, China, Brazil na Urusi ni kati ya nchi zilizopiga kura kupinga mapendekezo hayo.

Uamuzi huo wa UN ni matokeo ya kuidhinisha mapendekezo yaliyowasilihwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), Jumataano wiki hii, ikiitaka kuiondoa bangi katika orodha ya jedwali la IV la maazimio ya UN kuhusu madawa yanayoathiri ubongo na tabia ambayo sio tiba.

Jedwari la IV ni vitu ambavyo vinachukuliwa kama huleta ulaibu wa kiwango cha juu, kuharibu afya ya akili kwa kiwango cha juu na madhara mengine. Bangi ilikuwa kwenye orodha sawa na madawa ya kulevya aina ya cocaine na heroine.

Hata hivyo, imeendelea kuiweka bangi katika orodha yake ya Jedwari la I ambayo ni ya vitu ambavyo haviruhusiwi kutumika.

Makundi ya watu wanaounga mkono matumizi ya bangi kwa maelekezo ya daktari kama chanzo cha tiba limeonesha kufurahishwa na hatua hiyo. Reuters, imewakariri, “hii ni habari njema kwa mamilioni ya watu ambao wanatumia mmea huu kwa ajili ya matibabu na inaakisi uhalisia wa ukuaji wa soko lake.”

Angalizo ni kwamba uamuzi huo wa UN hautakuwa na madhara yoyote kwa sheria na taratibu za Serikali duniani kwa wakati huu kuhusu udhibiti wa bangi kama madawa ya kulevya. Kwani bado nayo imeiweka katika orodha ya vitu visivyotakiwa kutumika.

Lakini itaongeza jitihada kwa ya kuhalalisha matumizi ya mmea huo kama tiba kwa nchi ambazo zilikuwa zinasubiri muongozo wa UN katika suala hilo.

*Endelea kuzingatia sheria ya nchi yako.

Masau Bwire amkosoa Haji Manara
Ronaldo kidume, aweka rekodi mpya Ulaya