Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kuachiwa mara moja kwa watu 30, wa chama kikuu cha upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutoka rumande ili waendelee na shughuli zao za kisiasa na za kila siku.

Wanachama wa vyama vya Union for Democracy na wenzao wa Social Progress, walikamatwa siku ya Jumapili katika mji wa Lubumbashi, ulioko Kusini mashariki mwa nchi hiyo, baada ya polisi kusambaratisha mkutano wao.

Aidha, utawala wa Rais wa nchi hiyo, Joseph Kabila umepiga marufuku mkutano wa aina yoyote wa kisiasa pamoja na maandamano ya upinzani, tangu muda wake wa kukaa madarakani ulipoisha kisheri mwaka mmoja uliopita.

Tume ya uchaguzi nchini humo imesema kuwa haitakuwa rahisi kuandaa uchaguzi mkuu wa Urais, kabla ya mwezi Aprili mwaka ujao kwani hali ya kisiasa bado ni tete nchini humo hasa baada ya kuzuiwa kwa mikutano ya hadhara.

Hata hivyo, Chama kingine cha upinzani- Union for the Congolese Nation, kimesema kuwa, kitajiondoa katika serikali ya ugawanaji mamlaka, kuhusiana na kucheleweshwa kwa uchaguzi mkuu.

Video: Lulu akana kusababisha kifo cha Kanumba, Uteuzi wa Gavana mpya watikisa
Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 24, 2017