Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umetahadharisha kuhusu mzozo wa kisiasa nchini humo uliochochewa na hatua ya rais Felix Tshisekedi kuuvunja Muungano kati ya vyama tiifu kwake na rais wa zamani Joseph Kabila.

Umoja wa Mataifa umeonya kwamba huenda hatua hiyo ikaathiri uchumi wa taifa hilo na hali ya kiusalama iwapo hautasuluhishwa.

Kiongozi wa ujumbe huo nchini Congo, Leila Zerrougui ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba hatua hiyo inaweza kuwa na athari kubwa na kuchochea kufikiwa kwa makubaliano yatakayotanguliza maslahi ya watu wa Congo, kabla ya malengo ya muda mfupi ya kisiasa ambayo yanaweza kuongeza wasiwasi.

Wanachama 15 wa Baraza hilo walifanya kikao cha ndani baada ya taarifa hiyo, lakini halikuchukua hatua zozote za haraka na wala halikutoa taarifa yoyote.

Mamia ya watu wanaounga mkono Rais Tshisekedi wameelezwa kufurahishwa na  Tamko la kuvunja Muungano wa Cash- FCC kati ya Tshisekedi na mtangulizi wake Kabila.

Lwanga kamiligado Simba SC
KMC FC yaisukia mipango Mtibwa Sugar