Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kusimamishwa kwa muda mapigano katika mji wa Ragga nchini Syria, ili kuruhusu idadi raia waliopo katika eneo hilo la mapigano kuondoka kwaajili ya kuokoa maisha yao.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa misaada ya kibinadamu nchini Syria, Jan Egeland, ambapo amesema kuwa mji wa Raqqa umekuwa ni moja ya maeneo hatari sana nchini humo ambayo kila siku yamekuwa yakigharimu maisha ya watu kutokana mapigano makali ambayo yanaendelea hivi sasa.
Amesema kuwa hatua za haraka zinahitajika kuchukuliwa ili kuweza kutoa mwanya kwa raia wanaoishi katika mji huo kuweza kuondoka kwani wamekuwa wakiangamia kila kukicha.
Aidha, ameongeza kuwa wapiganaji wa Islamic State wanatumia kundi la raia waliobaki katika mji huo kama kinga ya kivita, ambapo inakadiriwa kuwa kuna idadi ya raia takribani 2,5000 waliokwama ndani ya mji huo huku kukiwepo mashambulizi ya mfululizo.
-
Rais Maduro akabiliwa na tuhuma za rushwa
-
Korea Kaskazini yazidi kuivuruga Marekani.
-
Vita ya Syria yazidi kuangamiza mamia ya raia
Hata hivyo, Marekani na Muungano wa vikosi vya Syria, Kiarabu na Kikurdi wanajaribu kuukomboa mji huo kutoka mikononi mwa wapiganaji wa Islamic state ambao wameweka ngome yao kubwa katika mji huo.