Kwa kawaida Mwanaume unapohitaji kuanza uhusiano na msichana unaempenda sana, kiu na njaa ya kuwa naye huwa iko katika kiwango kisichopimika.

Hasa unapokuwa unaanza kuwasiliana nae na ukafanikiwa kumsogeza karibu na kumuonesha kwa vitendo kuwa unampenda na kwa bahati nzuri, akaanza kukuwashia ‘Taa ya Kijani’.

Hata hivyo, mwanzo huu unaweza kuwa mbaya kwako endapo hautazingatia kanuni moja muhimu sana kati ya kanuni nyingi za kuendeleza na kudumisha mapenzi yaliyochipua yanayohitaji mbolea na maji safi kutoka kwako ili yachanue.

Ingawa ukweli ni kwamba muonekano wake na mvuto alionao mwanamke unaempenda unaweza kuwa ndio chanzo kikubwa kilichokusukuma kumfuata na kuanzisha maongezi kwa mara ya kwanza, ni muhimu sana kutomuonesha dalili zozote kuwa ‘ngono’ ndio hitaji lako la kwanza au kitu ulichokipa kipaumbele.

Kabla hujamwambia kitu chochote, kumbuka yule ni mtu mzima, mrembo aliyewavutia wengi kabla yako. Jiulize maswali kadhaa, je, kwa makadirio ya haraka haraka unadhani kuna neno jipya utakalomwambia ili akuamini wewe tofauti na wanaume wengine waliowahi kuongoa naye?

Hapo ndipo utagundua kuwa maneno yako yana nafasi ndogo sana kwake hivyo unapaswa kuyachagua kwa umakini mkubwa ili yapenye masikio yake na kuyahifadhi kwa muda ili ayatafakari kabla hayauruhusu moyo wake kuyatafrisi.

Wataalam wa masuala ya mahusiano wanashauri kuwa lugha ya mwili (body language) inaongea kwa sauti zaidi ya sauti yako. Hivyo, unapaswa kujiweka vizuri tangu unapomuangalia, unapomsalimia, mwili wako unapaswa kuongea kitu.

Hii inakuwa rahisi sana kama moyo wako umempenda kweli, mwili huongea wenyewe bila kuulazimisha.

Wanawake wengi wanajua kuzisoma lugha za mwili hata kabla ya lugha ya sauti. Hata hivyo, mioyo yao huwa migumu kuamini kile wanachokiona au kukisikia hususan kama wameshawahi kuumizwa mara kadhaa (kitu ambacho kipo kwa wanawake wengi hasa warembo).

Hata hivyo, baadhi hujikuta wanakupa nafasi ya kukusikiliza baada ya kugundua kuwa wewe unaonesha kupenda kweli tangu machoni. Imani ambayo huwepo kwa muda tu huku wasiwasi wa kuwa huenda unadanganya unakuwa juu zaidi.

Maneno na vitendo vyako vitakusaidia sana katika kuuteka moyo wa msichana unaetaka kuanzisha nae uhusiano ‘serious’ hivyo yachague kwa umakini. Tumia muda fulani mdogo kumsoma anachopenda, story anazopenda kuongelea na sehemu anazopenda kutembelea. Fahamu pia aina ya filamu anazopendelea na mengine ili uweze kuwa aina ya mwanaume unayeweza kucheza kila ngoma atakayokupigia katika mtiririko wa maisha.

Utafiti huo utakurahisishia maisha, na endapo utakaa naye vizuri na uhusiano wenu unaweza kuanza hata bila kumwambia maneno mengi. Yaani vitendo vikaongea hata bila kutumia maneno yanayotafsirika kama ‘kutongoza’. Kitakachofuata ni kumwambia maneno machache ili asikie alichokuwa anataka kusikia kutoka kwako. Funguka, na mwambie kiunaga ubaka.

Lovers

Nini cha kufanya baada ya kukubaliwa kuwa wapenzi?

Kama sio mpitaji kwake, na unataka uhusiano wenu uwe ‘Serious’, usikurupuke kuanza kumuomba kukutana nae katika sehemu ambazo zinatoa picha ya wazi kuwa unatengeneza mazingira ya kufanya nae ngono. Jitahidi kumfanya aone unamhitaji yeye na sio ngono.

Kumbuka katika kipindi hiki, kama ni mwanamke mwenye akili na anaetaka uhusiano ‘serious’ kila unachofanya au unachoongea kwake kina maana kubwa na anakuchorea picha ya maisha yenu ya baadae katika ubongo wake.

Kuwa mvumilivu, tengeneza uhusiano wa kwanza kama urafiki uliopitiliza na muoneshe kujali na kumpenda sana kisha mengine yatatiririka kwenye mkondo huo hadi mtakapoanza maisha ya Uchumba na kufikia hatua ya Ndoa.

Usimpoteze mkeo mtarajiwa kwa kuonesha kiu ya ngono zaidi ya kiu ya kuwa naye kama mpenzi unaetaka kufanya nae maisha.

Angalizo: Kwa bahati mbaya, baadhi ya wanaume hutumia mbinu hii kufanya maigizo ya kumnasa msichana ambaye kiuhalisia unaweza kukuta anamhitaji kwa ajili ya ‘Ngono’ tu lakini antigiza yote hata miaka kadhaa ili kumnasa.

Matokeo yake mapenzi haya huwa shubiri baada ya muda mfupi na kumuacha msichana aliyenasa bila kujua akiwa na majonzi makubwa. Huu ni ukatili wa kisaikolojia ambao mwanaume yeyote lijari anapaswa kuufikiria kwa kuwa unaweza kugeuka kuwa ugonjwa utakaomtesa mwenzi wake na hata kupelekea kuwaza kujiua.

Ili kuepuka athari kubwa ambayo unawez kuisababisha, ni vyema ukausikiliza kwanza moyo wako kama unataka kuingia kweli kwenye uhusiano serious na msichana kabla ya kufanya hivyo. Kumbuka mapenzi ni uwanja mpana zaidi ya ngono. Kuwa mkweli tangu unapoanza mahusiano.

 

Chup* Ya Gwajima Yatinga Mahakamani Kama Ushahidi
Ray C: Najua Mpango Wao Ni Kuniua