Mlinda Lango wa Athletic Bilbao, Unai Simon amefichua kwamba, katika wachezaji ambao amekutana nao hatari baada ya Lionel Messi ni Karim Benzema aliyekuwa Real Madrid.

Unai ambaye ni Mlinda Lacho chaguo la kwanza wa Bilbao, amebahatika kukutana na mastaa hao wawili katika michezo tofauti ya La Liga na Copa del Rey.

Kipa huyo amesema amekuwa akimpenda zaidi Benzema kutokana na ubora wake japo Messi alimsumbua sana kipindi wanakutana La Liga.

“Benzema ni kati ya wachezaji ambao ninampenda namna anavyocheza, ni mchezaji ambaye alikuwa akinipa wakati mgumu zaidi hasa baada ya Messi kuondoka maana naye wakati wake ndiyo alikuwa hatari zaidi,” amesema kipa huyo.

Unai Simon na Karim Benzema

Benzema msimu ujao hatakuwa ndani ya La Liga, baada ya kujiunga na Al-Ittihad ya Saudi Arabia, huku Messi yeye atakuwa Inter Miami.

Aliondoka La Liga misimu miwili iliyopita akitua Ufaransa kunako kikosi cha PSG.

Joash Onyango awekewa ngumu Simba SC
Ahmed Ally: Tutawatambulisha wachezaji wa kazi