Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) na linalo shughulikia wakimbizi (UNHCR), limeitahadharisha Marekani kuwa iko katika ukingo wa kukiuka sheria za kimataifa kwa kuwazuia watu wanaohitaji hifadhi nchini humo.
Wakati huo huo karibu watu elfu tatu wamezuiliwa kwenye mpaka kati ya Mexico na Guatemala, huku shirika hilo linaendelea kusisitiza kuwa watu wanaokimbia unyanyasaji na uvunjifu wa amani wanahaki ya kulindwa kimataifa
Aidha, kauli hiyo inakuja mara baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump kuzitishia nchi za Mexico na Hondurus kwamba Marekani itasitisha misaada yake kwa nchi hizo.
Kwa upande wa Marais wa Hondurus na Guatemala walikutana mwishoni mwa wiki iliyopita, Guatemala City kuzungumzia tatizo hilo na Rais wa Guetamala, Jimmy Morales akiwa pamoja na mwenzake, Juan Orlando wa Hondurus amesema watu elfu mbili tayari wamesharudi nyumbani.
-
Video: Muonekano wa ndani ya ndege ya kifahari zaidi duniani
-
Trump avalia njuga mauaji ya mwandishi Saudi Arabia
-
Trump, Putin kuteta jijini Paris
Mfanyakazi wa shirika linalo hudumia wahamiaji (UNHCR), Flor Cedrel amesema kuwa watu hao wanahangaika kwakuwa hawaruhusiwi kuingia Marekani.