Wakati jitihada zikifanyika kukabiliana na vitendo vya vipigo na unyanyasaji wa kingono kwa wanawake, kwa sasa mitandao ya kijamii imekuwa changamoto kubwa kwa wasichana.

Hayo yamesemwa na Mtetezi wa haki za binadamu na wanasheria Anagrace Rwehumbiza, wakati akizungumza na mabinti katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Ambapo amesema kuwa baadh ya watu wamekuwa wakitumia vibaya mitandao hiyo kwa kuwadhalilisha wanawake na wasichana kwa kuwekwa picha chafu na video zao za faragha.

“Mabinti wanakumbana na udhalilishaji huu, lakini jamii haioni kama ni tatizo ndio kwanza wanashiriki kusaka kuziona hizo picha badala ya kupambana na wanaozisambaza” amesema Rwehumbiza

Hata hivyo amesema kuwa sheria ya makosa ya mtandao haitaweza kufanya kazi kukabiliana na ukatili wa kijinsi mitandaoni endapo jamii haitoona kuwa hilo ni tatizo kubwa na kutoa taarifa kwa vyombo husika .

Ronaldo kidume, aweka rekodi mpya Ulaya
Mwinyi apinga Corona kuwa kisingizio ukusanyaji kodi