Kocha Mkuu wa Mashujaa FC, Mohamed Abdallah ‘Baresi’ amekalia kuti kavu baada ya mashabiki wa timu hiyo kuushinikiza uongozi wa timu kumfukuza kutokana na uwenendo mbaya wa timu hiyo.
Mashujaa juzi Jumanne (Desemba 05) ililazimishwa sare va bao 1-1 na Tabora United ikiwa nyumbani Uwanja wa Lake Tanganvika matokeo anbayo yalizidi kuiweka tinu hiyo katika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na pointi tisa.
Mwenyekiti wa timu hiyo, Maja Mgaya amesema pamoja na shinikizo la mashabiki hao lakini bado wanainani na Baresi anaweza kubadili upepo na kuwapa matokeo mazuri kwenye mechi zijazo.
“Ni kweli tupo nafasi mbaya sababu hatujapata ushindi katika mechi nyingi tulizocheza karibuni, tuna mpango wa kukutana na benchi la ufundi kujua nini tatizo baada ya hapo tutajua cha kufanya” amesema Mgaya.
Amesema uongozi hawafurahishwi na mwenendo wa tinu yao lakini hawawezi kukurupuka kwa kufanya maamuzi ambayo huenda yakawagharimu mbeleni.
Amesema bado wanatoa nafasi kwa Baresi na wenzake lakini pia wanaangalia uwezekano wa kuboresha kikosi chao kwa kuongeza wachezaji wenye uzoefu ili kupata matokeo mazuri zaidi.