Mwenyekiti wa Simba SC Murtaza Mangungu amemkingia kifua Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo Barbara Gonzalez, ambaye kwa asilimia kubwa anapigwa vita na baadhi ya wadau wa klabu hiyo.
Barbara amekua akitajwa kama kiongozi anayekwamisha maendeleo ndani ya Simba SC, nah ii ilidhihirika baada ya kuondoka kwa aliyekua Mkuu wa Idara ya Habari na Mwasilino klabu hapo Haji Manara na baadae Kassim Dewji alimtaja mwanadada huyo alipohojiwa na kituo cha EFM mapema mwezi uliopita.
Mbali na wawili hao kumtuhumu Barbara, pia Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Bernard Morrison amemtaja kiongozi huyo kama chanzo cha yeye kuondoka Simba SC, hasa baada ya kugoma kusaini mkataba mpya ambao amedai ulikua na maslahi madogo.
Magungu amesema Uongozi wa Simba umekua ukisikia mlalamiko na dhihaka nyingi dhidi ya Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, lakini kila alishiriki kumtuhumu akiombwa Ushahidi amekuwa hauniki hadharani.
Akihojiwa na EFM mapema leo Ijumaa (Julai Mosi), Mangungu alisema: “Unaposema Barbara ana mapungufu tueleze mapungufu yapi? Sasa unasema ana mapungufu na husemi tutajuaje? Kama Morrison anasema hakuridhishwa zipo sehemu za kufuata kuna TFF, Chama Cha Wachezaji, kuna CAF na mpaka FIFA. Na mkataba ni wa pande mbili, Kuna pande ya mchezaji (Morrison) na upande wa Simba”
“Barbara Gonzalez ni mtekelezaji wa maagizo ya bodi…Barbara hafanyi Kwa maamuzi yake, Kila anachosimamia yeye ni maamuzi ya bodi. Wanaomlaumu huenda wanamlaumu kutoka na hali yake (Jinsia).”
“Kama tutampima kwa mfanikio yake Barbara kafaulu sana. Ubingwa wa ligi, Ubingwa wa ASFC na hata kimataifa kafanya vizuri. Kwenye biashara ya Wachezaji Simba imeuza pia Wachezaji (Chama, Miquissone, Bwalya). Msimu huu hatukuwa vizuri kama utasema hatoshi kutokana na msimu huu kuwa mbaya sio sahihi, Kwa sababu kuna up and down.”