Uongozi wa timu ya Simba ukiongozwa na Rais wa timu hiyo, Evans Aveva leo umekutana na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe katika Ofisi zake Mjini Dodoma.
Uongozi wa Simba umeitikia wito wa Dkt. Mwakyembe wa kukutana naye ili waweze kujadili masuala mbalimbali ya mpira wa Miguu zikiwemo fursa na changamoto katika mabadiliko na maendeleo ya mpira na uendeshaji wa timu hapa nchini.
Aidha, Katika hatua nyingine Mwakyembe amepokea maoni ya Uongozi wa Simba na kushauri kuendelea kutoa ushirikiano na wadau wa mpira wa miguu.
Hata hivyo, Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Prof. Elisante Ole Gabriel, Mkurugenzi wa Michezo Yusufu Omary, Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja, na Msajili wa Vilabu na Vyama hapa nchini