Taarifa zilizosambaa mitandaoni wiki hii kuhusu hali tete ya kiafya ya mwanamuziki wa Nigeria, 2Face Idibia ambaye sasa anajiita 2Baba zimeuibua uongozi wake na kuweka mambo sawa.

Kulikuwa na taarifa kuwa msanii huyo alikuwa katika hali mbaya na amelazwa hospitalini. Taarifa hizo ziliendelea kudai kuwa 2Baba alihudhuria mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya kutimiza masharti ya mkataba wake na ‘Nigerian Stock Exchange’.

“Alitoka hospitalini kuhudhuria mkutano kwa sababu za kuhakikisha anakidhi vigezo vya mkataba wake, lakini alikimbizwa tena hospitalini baada tu ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari,” taarifa hiyo ilieleza.

Hata hivyo, chombo cha habari cha E-Day cha Nigeria kilizungumza na uongozi wa mkali huyo wa ‘African Queen’ na ulikanusha taarifa hizo.

Kwa mujibu wa E-Day, mmoja wa viongozi wa 2Baba alieleza kuwa msanii huyo yuko katika hali nzuri ya kiafya na hajawahi kulazwa hospitalini hivi karibuni.

Trump akutana na wahanga wa mashambulizi ya Dayton na El Paso, Mamia waandamana
‘Yesu feki’ wa Kenya hajafa, aonekana tena mitaani, afunguka