Makamu wa Rais wa klabu ya Young Africans Arafat Haji, amewaondoa wasiwasi Mashabiki na Wanachama wa Klabu hiyo kuhusu mustakabali wa Mshambuliaji kutoka DR Congo Fiston Kalala Mayele, ambaye anadaiwa kuwindwa na baadhi ya Klabu za BArani Afrika.

Kufanya vizuri kwa Mayele akiwa na Young Africans kwenye Michuano ya Kimataifa kumezitamanisha klabu kadhaa kuhitaji huduma ya Mshambuliaji huyo ambaye amekuwa msaada mkubwa kwa Wananchi.

Baadhi ya klabu zinazotajwa kuwania saini ya Mshambuliaji huyo kinara wa mabao katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu huu akifunga saba ni Kaizer Chiefs, Orlando Pirates za Afrika Kusini, US Berkane na Raja Casablanca za Morocco.

Arafat amesema wanafahamu klabu hizo zina fedha, ambazo anaamini Yanga pia wanazo za kutosha za kumzuia Mayele kuondoka.

Arafat amesema mshambuliaji huyo hivi karibuni aliongeza mkataba wa mwaka mmoja ambao unatarajiwa kumalizika rasmi msimu wa 2023/24.

Ameongeza kuwa, mkataba huo ukielekea kumalizika, uongozi umepanga kumuongezea mwingine wa kubakia kuendelea kuichezea Young Africans.

“Kama sababu ikiwa ni fedha Mayele ataondoka, basi niwaambie kuwa sisi pia Young Africans tuna fedha za kutosha kumpa ili abaki kuendelea kuichezea timu yetu.

“Fedha ndiyo inayotajwa kuwa Mayele zitamuondoa Young Africans, kama sababu ikiwa ndio hiyo basi wasahau kuondoka na badala yake atabaki hapa, kama ni fedha zipo za kutosha, hatutakubali kumuachia aondoke.

“Kwa ubora na kiwango hiki ambacho amekionesha ngumu kwetu kumuachia aondoke kwani kwa sasa tunatengeneza kikosi bora kitakachofanya zaidi kimataifa,” amesema Arafat

Chongolo ampa maagizo Bashe skimu ya umwagiliaji
Kipigo cha USMA, Kocha Nabi aitaja TFF, TPLB