Uongozi  wa klabu ya Young Africans umethibitisha kusimamishwa kwa wachezaji watatu wa klabu hiyo, na kuondolewa kambini ili kupisha taratibu za uchunguzi na kisha kutolewa kwa adhabu.

Young Africans wamethibitisha taarifa hizo kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii, ambapo wameweka wazi sababu ya nyota wao watatu “watukutu”; Metacha Mnata, Michael Sarpong na Lamine Moro kukosekana katika baadhi ya michezo kufuatia utovu wa nidhanmu.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, beki kutoka nchini Ghana Lamine Moro awali aliondolewa katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Namungo FC walipocheza mkoani Lindi, alirejeshwa Dar es salaam huku wakisema amerejeshwa akiwa anaumwa.

Upande wa Sarpong inaelezwa yeye aligoma kusafiri na timu kwenda Dodoma hali iliyowafanya benchi la ufundi pamoja na uongozi kiujumla kumuweka katika orodha ya utovu wa nidhamu.

Wakati huo huo kipa Metacha Mnata ambaye alikuwa na timu kwenye mchezo dhidi ya (Namungo FC na JKT Tanzania) amerejeshwa jijini Dar es Salaam baada ya utovu wa nidhamu, huku tetesi zikieleza kuwa mlinda mlango huyo alilewa kupitiliza akiwa kambini.

Hata hivyo uongozi wa Young Africans haujasema lolote kuhusu hukumu za wachezaji hao zitasomwa lini, huku kaimu katibu mkuu CPA Haji Mfikirwa aliwahi kuthitibisha taarifa za beki Lamine Moro kuwa mbini kuitwa mbele ya kamati ya nidhamu ili ajitetee.

IGP Sirro aonya wanaoajiri walinzi wazee
Mwinyi ateua Mkuu wa Shule ya Sheria ZNZ