Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari Nnauye Nape ameiagiza TCRA kuyaagiza makampuni ya simu kusitisha upandishaji wa bei ya Vifurushi mpaka hapo watakapokaa na Serikali kuzungumza kuhusu jambo hilo.


Hii imekuja ikiwa ni siku chache tangu wananchi kuanza kulalamikia kuwa bei za vifurushi vya simu zimepanda ghalfa na huku wengine wakienda mbali zaidi na kudai kuwa kiwango cha vifurushi wanachopewa wakinunua hakiendani na bei halali wanayokuwa wamekatwa.


“Kuna gharama kidogo zimeongezeka kwa baadhi ya kitandao ya simu, nikaanza kusikia kelele, tunataka mawasiliano yawe bora, rahisi na ya kisasa. Tukiweka mawasiliano halafu uwezo wa kuyatumia haupo, mtatuletea shida,” alisema

“Serikali inatambua hali ya upandaji wa kutoa huduma na kasi ya mahitaji ya Soko lakini kasi ya upandaji isiwe kubwa.” Aliongeza Nape.

Waziri Nape amewataka TCRA pamoja na makampuni ya simu kuhakikisha wanapandisha kwa utaratibu bei hizo huku wakiangalia urahisi na upatikanaji wa taarifa.

Waziri Bashungwa aanza na maagizo haya
Radi yaua watu zaidi ya watano.