Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kikosi cha usalama Barabarani, limewaonya baadhi ya mawakala wanaopandisha nauli kiholela kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kuwa halito wafumbia macho mawakala na wamiliki wa magari hayo.

Akiongea hii leo Decemba 13, 2022 jijini Arusha, Mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa Arusha mrakibu wa Polisi, Solomon Mwangilo amesema tiketi zinakatwa kwa mfumo wa kieletroniki na kuwataka wamiliki na wakala wa mabasi kufuata utaratibu na maelekezo ya serikali kwa ukataji tiketi kwa mfumo wa kieletroniki.

Amesema, hatua kali zitachukuliwa kwa wakala atakaye bainika kukiuka maagizo ya serikali na kwamba madereva wanapaswa kufuata sheria za usalama Barabarani, ili kuepusha ajali ambazo nimkuwa ziki ghalimu Maisha ya watu ambapo amebainisha kuwa Jeshi hilo halina ugomvi na madereva wanafuata sheria za usalama barabarani.

Nae Yahaya Mbwana ambaye Pia ni dereva wa basi linalofanya safari zake kati ya Singida na Arusha amewataka madereva wenzake kufuata sheria za usalama Barabarani ili kuepusha ajali ambazo chanzo chake ni ukikwaji wa sheria za usalama barabarani.

Kwa upande wao, baadhi ya mawakala wa mabasi yaendayo Mikoani wamesema changamoto kubwa kutoka kwa abiria wao ni uelewa mdogo juu ya mfumo mpya na bei elekezi ya serikali ambapo wamesema imekuwa chanzo cha malalamiko kwa abiria.

Mapacha tisa 'Guiness' warejea nyumbani salama
Kairuki mgeni rasmi kongamano ukatili kwa Watoto