Upanuzi wa migodi ya shaba na Cobalt nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC umechochea kuongezeka kwa ukiukwaji wa haki za binadamu.
Ripoti ya Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za Binaadamu la Amnesty International na lile la Kongo IBGDH imeyabani hayo na kusema jamii zinazoishi karibu na miji yenye migodi kama Kolwezi, hulazimishwa kuyahama makazi yao, ili kupisha miradi hiyo.
Katika Ripoti hiyo, kuna msisitizo kuwa watu hao wanapaswa kunufaika na uchimbaji wa madini hayo na kuwahamisha bila kujali athari watakazozipata na usumbufu wa ujenzi wa makazi mapya ikiwemo maeneo ya kufanya shughuli zao ni vitendo visivyofaa.
Katibu Mkuu wa Amnesty International, Agnes Callamard amesema Shirika hilo pia linatambua hitaji muhimu la kuelekea kwenye matumizi ya Nishati mbadala, lakini linalenga kukomesha vitendo vya dhuluma dhidi ya raia wanaoishi katika maeneo yanayogundulika kuwa na migodi.