Wakuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wa Mikoa, Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa, na Waendesha Mashtaka wa Mikoa wametakiwa kujenga utamaduni wa kushirikiana, ili kazi ya upatikanaji wa haki iweze kuendelea zaidi.

Wito huo, umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU, Kamishna wa Polisi, Salum Hamdun na kuongeza kuwa pia wanatakiwa kujishusha katika utendaji wao.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU, Kamishna wa Polisi, Salum Hamdun.

Aliyasema hayo wakati akifungua kikao Cha Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Ofisi ya Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kinachoendelea Jijini Dodoma.

Kikao hicho kimehusisha vyombo vyote vinavyohusika na haki jinai, ambavyo ni Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.

Mtumishi ukiajiriwa jipange na kustaafu - Kaganda
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Oktoba 1, 2023