Mkuu wa Gereza Kuu Ukonga, Kamishina Msaidizi wa Magereza, Dkt. Juma Mwaibako amelipongeza Jeshi la Polisi kwa jinsi linavyoishirikisha jamii katika kubaini, kutanzua na kuzuia uhalifu Nchini.

Kauli hiyo, ameitoa wakati akipokea misaada mbalimbali kutoka kwa Askari Polisi waliotimiza miaka nane ya utumishi ndani ya Jeshi hilo, ambapo amebainisha kuwa Jeshi hilo limebadilika sana kiutendaji ambao unaoendana na mabadiliko ya dunia.

Kwa upande wake Mwanafunzi wa Kozi ya Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Amosi Mikao amesema wametoa misaada hiyo ikiwa ni sehemu ya shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwalinda katika kazi zao.

Naye Mwanafunzi wa Kozi ya Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Rose Kitula amesema wameungana kulikumbuka kundi hilo lenye mchango katika jamii na Taifa kwa ujumla kiuchumi, kwa kuwasadia vifaa mbalimbali Gereza Kuu la Ukonga, jijini Dar es Salaam.

Serikali, Wadau kuikabili changamoto Afya ya akili
Wafanyabiashara washauriwa kufunga Kamera za ulinzi