Mustakabali wa mshambuliaji wa FC Barcelona aliyefunga bao lililoipa ubingwa klabu hiyo wa Uefa Super Cup usiku wa kuamkia jana huko mjini Tbilisi nchini Georgia, Pedro Rodrigues wa kuelekea Old Trafford yalipo makao makuu ya Man utd umeingia dosari.

Taarifa zilizotolewa na katibu wa kitengo cha ufundi huko Camp Nou, Robert Fernandez zimeleta utata wa kuondoka kwa Perdo kwenye klabu ya Barcelona ambayo imeonyesha bado inahitaji huduma yake.

Fernandez, amesema Pedro ameuthibitishia uongozi wa Fc Barcelona, anahitaji kusalia klabuni hapo na hana mpango tena wa kuondoka kama ilivyokua ikizungumzwa kabla ya mchezo wa kuwania Uefa Super Cup dhidi ya Sevilla.

Hata hivyo tangu taarifa hiyo ya katibu wa kitendo cha ufundi cha FC Barcelona ilipotolewa, Pedro hajazungumza lolote.

Wananchi Waandamana Kupinga Goli La Mkono Kwa Nape
Utovu Wa Nidhamu Wamuweka Pembeni Wanchope