Kiongozi  wa Azimio la Umoja, Raila Odinga amesema upinzani utatangaza mkakati mpya kuwashinikiza Wakenya kuikabili Serikali ya Kenya Kwanza, kutokana na uwepo wa gharama za juu za maisha.

Odinga amesema utendaji wa Serikali ya Rais William Ruto ni mbaya, licha ya kuelekea kumaliza mwaka mmoja madarakani, kwa umeshindwa kudhibiti bei ya mafuta na ushuru, hali ambayo imechangia kupanda kwa gharama ya maisha.

Odinga aliyekuwa ameandamana na Viongozi wenza katika mrengo huo, alisema tayari wamekusanya saini milioni 10 za Wakenya wanaopinga utawala wa Kenya Kwanza.

Kiongozi  wa Azimio la Umoja, Raila Odinga. Picha ya DN.

Aidha, amefafanua kuwa saini hizo ndizo zitakazotoa mwelekeo kuhusu hatua watakazochukuwa dhidi ya Serikali ya Ruto lakini hawatarejelea maandamano.

“Tutawazungumzia raia kuhusu masuala yanayowaathiri Wakenya. Kama mnavyojua, tumekuwa tukikusanya saini, ambapo zimetosha kwa sasa. Tunajua tutakachokifanya na saini hizo. Hatutawaambia watu kurejelea maandamano. Watarejea kufanya jambo jingine tofauti,” alisema Odinga.

Dkt. Mwinyi aitumia vyema falsafa ya uzalendo Kibiashara
Viongozi sikilizeni, tatueni kero za Wananchi - Rais Samia