Maandamano yaliyoitishwa na viongozi wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, (DRC), yameshindwa kupata mwitikio mkubwa kama ilivyotarajiwa baada ya Serikali kuyapiga marufuku na kusambaza maelfu ya polisi.

Maandamano hayo yalikuwa yanalenga kupinga kalenda mpya iliyotangazwa na Tume ya uchaguzi nchini humo, ambayo sasa inaonyesha kuwa uchaguzi mkuu utafanyika Disemba 23 mwaka 2018.

Aidha, Rais Kabila amemaliza muda wake wa kuiongoza nchi hiyo tangu Disemba 20 mwaka jana kabla ya kufikiwa kwa makubaliano kati ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki, na wanasiasa kuwa uchaguzi ungefanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Upinzani ulikuwa unajaribu kuwashawishi wafuasi wake kujitokeza kwa wingi kwenye viunga vya jiji la Kinshasa na maeneo mengine ya nchi kushinikiza Rais Joseph Kabila kuondoka madarakani ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

 

Hata hivyo, Upinzani umeendelea kushinikiza kuwa unataka kuundwa kwa Serikali ya mpito bila ya Rais Kabila kuanzia Januari Mosi mwaka 2018

Polisi wavamia shule ya Kiislamu
Magazeti ya Tanzania leo Desemba 20, 2017