Wagombea wa vyama vya upinzani katika uchaguzi mkuu nchini Uganda unaotarajiwa kufanyika Alhamisi hii nchini humo, wameazimia kushirikiana katika kulinda kura zao kwa pamoja.

Aidha, wamefafanua kuhusu mkakati wao wa kumuunga mkono mwenzao atakayepata kura nyingi ikiwa uchaguzi huo utaingia katika duru ya pili.

Mgombea wa Chama cha NUP, Robert Kyagulanyi maarufu kama, Bobi Wine, mgombea wa FDC, Patrick Oboi Amuriat na Jenerali Mugisha Muntu wa ANT wamesisitiza kwamba uchaguzi huu ni muhimu sana kwa Uganda na watafanya kila juhudi kulinda kura zao kwa pamoja.

Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari kuanza kutumika Januari 2022.

Hii ni kwa sababu wana imani kwamba Rais wa sasa Yoweri Museveni mara hii hawezi kupata asli mia 50 na kura moja ili kutangazwa mshindi wa duru ya kwanza.

Wagombea hao wamelezea kuwa ikiwa mmoja wao atapata kura nyingi na kulazimisha duru ya pili ya uchaguzi, wengibe wrote watamuunga mkono.

Odinga: Urais uwe wa makabila Kenya
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Januari 12, 2021