Jamii imetakiwa kuwalinda watoto dhidi ya ukatili unaotokana na urembo ambao umetajwa kuwa na madhara kiafya kwa watoto.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Doroth Gwajima wakati akizindua, kampeni maalumu itakayo walinda watoto dhidi ya ukatili wa urembo hapa nchini.
Waziri Gwajima pia amewataka wazazi kuacha tabia ya kuwaremba watoto kwa kuwavalisha na kuwaremba watoto vitu ambavyo haviendani na umri wao.
”Mtoto hata ukimfunga reboni tu inakka vizuri anapendeza lakini sio mtoto umembebesha mzigo wahereni, mwingine ana relaxa anamapunye huku mwingine unakuta anasukwa analia mpaka kapata homa kapewa panadol” amesema Waziri Gwajima.
‘Aidha Dkt. Gwajima amesema, ‘mimi nimekuwa nikipata vitu vingi nikijifunza vitu vingi na nimekuwa nikielemisha vitu vingi lakini nashukuru watu wamekuwa wakiendelea kuibua mijadala mahojiano mpaka tunafika mahala tunasema hizi mb zinaisha mwisho wake nini? nikisema njooni twende pamoja tutakwenda watu wamekuwa wakisema tutakwenda ”