Waziri Mkuu wa Ureno, Antonio Costa ametangaza siku tatu za maombolezo mara baada ya kutokea kwa janga la moto lililosababisha vifo vya watu 60 katika msitu uliopo katikati mwa nchi hiyo katika mji wa Pedrogao Grande.

Ameyasema hayo mara baada ya kutembelea eneo la tukio huku akiongeza kuwa kwa sasa moto umeshadhibitiwa kwa asilimia mia moja na jeshi la zima moto la nchi hiyo ambalo limekuwa likipambana usiku na mchana.

Amesema kuwa janga hilo ni kubwa kutokea nchini mwake kwa siku za hivi karibuni baada ya miaka kadhaa iliyopita kutokea kwa majanga ya mioto katika misitu mikubwa kama hiyo.

Umoja wa Ulaya, Ufaransa na Hispania vimejitolea kupeleka msaada wa ndege za kusaidia kuzima moto huo huku vikiahidi kushirikiana bega kwa bega na Ureno katika kutoa mahitaji yeyote ya kibinadamu.

 

Picha: Angalia Safari Ya Mwisho Ya Cheick Tiote
Florentino Perez Apeta Real Madrid