Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Uruguay imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali katika michuano ya Copa America baada ya ushindi mwembamba walio upata dhidi ya Chile.
Katika mechi baina ya Uruguay na Chile ambayo ilivuta hisia za watu wengi huku bao moja ambalo lilifungwa katika mchezo huo lilitosha kuivusha Uruguay kwenda hatua ya robo fainali huku washambuliaji wa Chile wakikosa nafasi ya kutikisa nyavu za wapinzani wao.
Mshambuliaji wa Uruguay Edson Cavan ambaye anakipiga katika klabu ya Paris Sant Germany ya nchini Ufaransa aliibuka shujaa wa mchezo huo na kwa kufunga goli hilo ambalo limeivusha timu ya taifa lake na kwenda robo fainali ambao pia kwenye mechi hiyo Cavan aliibuka mchezaji bora wa mchezo.
Baada ya mtanange huo Uruguay wamejichimbia kileleni kwa kufikisha alama saba kwenye msimamo wa kundi C, wakifuatiwa na Chile wenye alama 6 ambapo baada ya matokeo hayo timu mbili za Japan na Ecuador zikiwa zimefungasha vilago na kuaga mashindano hayo ambayo yanafanyika nchini Brazil.