Kikosi cha timu ya taifa ya Panama kinaingia nchini Urusi kikiwa kwenye meza ya mashambulizi ya Kundi G kikitarajiwa kula sahani moja na vikosi vya timu za taifa za Ubelgiji, Tunisia na Uingereza.

Panama inaingia kwenye mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia baada ya kutumia vizuri nafasi ya za kuwania kufuzu fainali hizi kupitia za ukanda wa Amerika ya kati na kaskazini (CONCACAF), ikianza kupambana katika mzunguuko wa nne.

Katika mzunguuko huo Panama walipangwa katika kundi B (Kundi La Pili) lililokua na timu za mataifa ya Costa Rica, Haiti na Jamaica.

Ilimaliza michezo ya kundi hilo ikishika nafasi ya pili kwa kufikisha alama 10, nyuma ya Costa Rica waliomaliza vinara kwa alama 16.

Panama na Costa Rica zilifuzu kwa hatua ya mzunguuko tano na kuwekwa kundi moja na mataifa mengine yaliyomaliza kwenye nafasi ya kwanza na ya pili (Kundi A na C).

Kwenye mshike mshike wa kundi la mzunguuko wa tano timu ya taifa ya Panama ilikuwa miongoni mwa mataifa matatu yaliyotakiwa kufuzu moja kwa moja kupitia ukanda wa CONCACAF, ikimaliza katika nafasi tatu baada ya kufikisha alama 13, ikitanguliwa na mataifa ya Costa Rica (Alama 16) na Mexico (Alama 21), huku taifa la Honduras likishika nafasi ya nne na kulazimika kucheza mchezo wa mtoano.

Majina ya utani ya timu ya taifa ya Panama: Los Canaleros (The Canal Men) na La Marea Roja (The Red Tide).

Mfumo: Kikosi cha Panama hutumia mfumo wa 4-4-2.

Related imageMchezaji Nyota: Gabriel Gómez (Atlético Bucaramanga)

Image result for Román Torres - panamaMchezaji hatari na Nahodha: Román Torres (Seattle Sounders)

Image result for Hernán Darío Gómez - panamaKocha: Hernán Darío Gómez (62), raia wa Colombia.

Ushiriki: Panama itashiriki kwa mara ya kwanza fainali za kombe la dunia mwaka huu 2018.

 

Kuelekea 2018:

“Tunakwenda katika fainali za kombe la dunia, kujifunza na kushindana. Itatusaidia kuongeza ujuzi na kufurahia mafanikio tulioyapata ya kucheza kwa mara ya kwanza katika michuano hii mikubwa duniani,” Aliwahi kusema kocha mkuu wa Panama Hernán Darío Gómez.

Kocha huyo kutoka nchini Colombia ameweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kuifikisha Panama katika fainali za kombe la dunia, na alichukua jukumu hilo kwa kukubali kujibebesha mzigo kama raia wa taifa hilo.

Gómez anaamini uwezo ulioonyesha na baadhi ya wachezaji wake wakati wakicheza michezo ya kuwania kufuzu, utaonekana kwa mara nyingine wakati wa fainali za mwaka huu zitakazoanza rasmi Juni 14 nchini Urusi.

Mchezaji hodari kikosini mwake ni Román Torres aliefunga bao muhimu wakati wa mchezo wa mwisho wa kuwania kufuzu dhidi ya Costa Rica waliokubali kibano cha mabao mawili kwa moja, na kukata tiketi ya kushiriki kwa mara ya kwanza fainali za kombe la dunia.

Wengine ni Gabriel Gómez, Alberto Quintero, Gabriel Torres, Blas Pérez, Fidel Escobar, Michael Murillo na  Ismael Díaz.

Panama wataanza kampeni za kuusaka ubingwa wa mwaka huu kwa kucheza dhidi ya Ubelgiji, Uwanja wa Fisht Olympic mjini Sochi Juni 18, kisha watapambana na England Juni 23, Uwanja wa Nizhny Novgorod mjini Nizhny Novgorod, na mchezo wao wa mwisho hatua ya makundi watakutana na Tunisia Juni 28, Mordovia mjini Saransk.

Kaa nasi, Dar24 kesho tutamulika timu nyingine na huu ni muendelezo hadi nyasi za Urusi zitakapoanza kupata joto la mitanange ya fainali hizo.

Simba: Ni lazima tukawachape Everton, Gor Mahia hawana kitu
Video: Harmorapa afunguka kutoswa na Meneja wake