Sweden imepangwa katika kundi F lenye timu za Ujerumani, Mexico, Sweden na Korea Kusini.

Haikuwa kazi rahisi kwa Sweden kupata uhakika wa kushiriki fainali za kombe la dunia za 2018 ikitokea ukanda wa barani Ulaya, kwani iliwalazimu kusubiri hadi katika mchezo wa mtoano, baada ya kuamliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi A (kundi la Kwanza).

Sweden walifikisha alama 19 nyuma ya Ufaransa waliomaliza kileleni kwa alama 23, lakini walizishinda nchi nyingine zilizokuwa katika kundi hilo kama Uholanzi, Bulgaria, Luxembourg na Belarus.

Hata hivyo, kumaliza katika nafasi ya pili haikuonesha simanzi kwa wachezaji wa taifa hilo, kwani asilimia kubwa miongoni mwao walikuwa na matumaini ya kufanikisha safari ya kwenda Urusi kwa kumsubiri mpinzani waliopangiwa kwa ajili ya mchezo wa mtoano kupitia ukanda wa Ulaya.

Sweden walipangiwa kukutana na mabingwa wa soka duniani mwaka 1934, 1938, 1982 na 2006, timu ya taifa ya Italia.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya mtoano uliofanyika Friends Arena mjini Solna, Novemba 10, 2017, wenyeji Sweden walichomoza na ushidni wa bao moja kwa sifuri lililofungwa na kiungo Jakob Johansson.

Novemba 13, 2017 timu hizo zilicheza mchezo wa mkondo wa pili kwenye uwanja wa San Siro mjini Milan nchini Italia, na kumaliza dakika 90 kwa matokeo ya sare ya bila kufungana, hivyo moja kwa moja Sweden alikata tiketi ya kushiriki fainali za kombe la dunia za 2018 kwa jumla ya ushindi wa bao moja kwa sifuri.

Jina la utani la timu ya taifa ya Sweden: Blågult (The Blue-Yellow)

Mfumo: Kikosi cha Sweden hutumia mfumo wa 4-4-2.

Image result for Emil Forsberg - swedenMchezaji Nyota: Emil Forsberg (RB Leipzig)

Related imageMchezaji hatari: Viktor Claesson (Krasnodar)

Image result for Andreas Granqvist - swedenNahodha: Andreas Granqvist (Helsingborgs IF).

Image result for Janne AnderssonKocha: Janne Andersson (55), raia wa Sweden.

Ushiriki: Sweden imeshiriki fainali za kombe la dunia mara kumi na moja (11). Mwaka 1934, 1938, 1950, 1958, 1970, 1974, 1978, 1990, 1994, 2002 na 2006.

Mafanikio: Mshindi wa pili (1958).

Kuelekea 2018:

Mwaka 2016 wakati wa fainali za mataifa ya Ulaya zilizofanyika nchini Ufaransa, Sweden ilikuwa ni mara ya mwisho kumtumia mshambuliaji woa hatari Zlatan Ibrahimovic ambaye alitangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa.

Mashabiki wengi nchini humo hawakuamini kama taifa lao lenye watu zaidi ya 10,142,686 kama lingeweza kufanya vyema katika michezo ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia, kwa kuwatumia baadhi ya wachezaji ambao hawakuwa na uzoefu.

Kwa maelezo nilioyatoa hapo juu imedhihirisha wachezaji walioaniwa na kocha Janne Andersson, walifuta mawazo kinzani ya mashabiki hao na kuipeleka timu katika fainali za kwanza tangu mwaka 2006.

Sweden wataanza kampeni za kuusaka ubingwa wa mwaka huu kwa kucheza dhidi ya Korea Kusini, Uwanja wa Nizhny Novgorod mjini Nizhny Novgorod Juni 17, kisha watapambana na mabingwa watetezi Ujerumani Juni 23, Uwanja wa Fisht Olympic mjini Sochi, na mchezo wao wa mwisho hatua ya makundi watakutana na Mexico Juni 27, Uwanja Central mjini Yekaterinburg.

Kaa nasi, Dar24 kesho tutamulika timu nyingine na huu ni muendelezo hadi nyasi za Urusi zitakapoanza kupata joto la mitanange ya fainali hizo.

Kampuni ya Emirate yazindua Ndege isiyokuwa na madirisha
Dkt. Tulia apangua hoja ya KKKT bungeni