Uruguay wamefuzu fainali za kombe la dunia 2018, wakitokea ukanda wa Amerika ya kusini ambapo mataifa yote hupangwa katika kundi moja, na mshindi wa kwanza hadi wa nane huingia moja kwa moja katika fainali hizo. Mshindi wa tano husubiri ili kucheza mchezo wa mtoano na timu kutoka ukanda wa Oceania.

Katika kundi la Amerika kusini, Uruguay walimaliza katika nafasi ya pili kwa kupata alama 31, nyuma ya Brazil waliokuwa vinara waliomiliki alama 41.

Majina ya utani ya timu ya taifa ya Uruguay: La Celeste (The Sky Blue), Los Charrúas (The Charrúa) na La Garra Charrúa (The Charrúa Claw).

Mfumo: Kikosi cha Uruguay hutumia mfumo wa 4-4-2.

Image result for luis suarez - uruguayMchezaji Nyota: Luis Suárez (Barcelona).

Image result for Federico ValverdeMchezaji hatari: Federico Valverde (Anacheza Deportivo La Coruña kwa mkopo akitokea Real Madrid).

Image result for Diego GodínNahodha: Diego Godín

Image result for Óscar TabárezKocha: Óscar Tabárez (71), raia wa Uruguay.

 

Ushiriki: Uruguay wameshiriki fainali za kombe la dunia mara kumi na mbili, hivyo nii ni mara ya kumi na tatu (13).  Walishiriki mwaka 1930, 1950, 1954, 1962, 1966, 1970, 1974, 1986, 1990, 2002, 2010 na 2014.

Mafanikio: Wanahistoria ya kipekee ya kutwaa kombe la dunia, mwaka 1930, wakati fainali za kwanza zilizochezwa nchini kwao. Uruguay ilitwaa ubingwa baada ya kuifunga Argentina mabao 4-2.

Mwaka 1950, ilitwaa tena ubingwa kwa mara ya pili ikiwanyang’anya tonge mdomoni Brazili waliokuwa wenyeji kwa magoli 2-1.

 Katika fainali za mwaka huu 2018, Uruguay ilipata nafasi ya kufuzu moja kwa moja, baada ya kupitia hatua ngumu ya kufuzu kwa kucheza mchezo wa mtoano dhidi ya mshindi kutoka Oceania, katika fainali nne mfululizo zilizopita.

Mafanikio hayo yalikuwa makubwa kwa kocha Tabarez ambaye aliajiriwa kukinoa kikosi cha Uruguay tangu mwaka 2006.

Kocha huyo hupendelea sana mfumo wa kushambulia wakati wote, na mwaka huu anatarajiwa kutumia mfumo huo ili kuifikisha mbali timu yake, baada ya mwaka 2014 kuondoshwa kwenye hatua ya mtoano (16 Bora).

Wachezaji wanaotegemewa na babu huyo ni kiungo mkabaji Federico Valverde anayecheza kwa mkopo Deportivo La Coruña akitokea Real Madrid, Matías Vecino (Internazionale), Nahitan Nández (Boca Juniors) na Rodrigo Bentancur (Juventus).

Uruguay imepangwa katika kundi la kwanza sambamba na wenyeji wa fainali hizo Urusi, Saudi Arabia na Misri.

Itaanza kampeni za kuusaka ubingwa mwaka huu kwa kucheza dhidi ya Misri katika Uwanja wa Central mjini Yekaterinburg Juni 15, kisha watapambana na Saudi Arabia Juni 20, Uwanja wa Rostov, mjini Rostov-on-Don, na mchezo wa mwisho watapapatuana na wenyeji Urusi Juni 25, uwanja wa Cosmos, mjini Samara.

Kutokana na kuwa na historia ya kutwaa ubingwa katika fainali hizi tena kwa kutoa kichapo kwa Argentina na Brazil kwa miaka tofauti, Uruguay inaweza kuwekwa katika timu zenye matarajio ya kuwa tishio kwa timu zote zinazoshiriki fainali za mwaka huu.

Wang’oa nyasi kwa mguu wakisaka ushindi katika kikosi hicho, wanatarajiwa kuwa Luis Suarez na Federico Valverde ambao wasifu wao katika ulimwengu wa Soka unawapa misuli ya kuwa tishio.

Suarez (31), anatazamiwa kuwa mchezaji ambaye atakua amejirekebisha kutokana na utovu wa nidhamu alioufanya wakati wa fainali za kombe la dunia 2014, amba ulipelekea kufungiwa miezi minne na shirikisho la soka duniani FIFA, baada ya kuthibitika alimng’ata beki wa Italia Giorgio Chiellini.

Mwaka huu anakwenda kwenye fainali za kombe la dunia akiwa hana skendo yoyote mbaya ya utovu wa nidhamu, baada ya kuitumikia vyema FC Barcelona na kuwa sehemu ya wachezaji walioiwezesha klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Hispania msimu wa 2017/18.

Amefunga mabao 25 katika ligi ya Hispania katika michezo 31 aliocheza ambazo ni sawa na dakika 2812. Upande wa ligi ya mabingwa msimu wa 2017/18, ambapo FC Barcelona waliishia hatua ya robo fainali, Suarez amefunga bao moja katika michezo 10 aliocheza ambayo ni sawa na dakika 884.

Endelea kufuatilia mfululizo wa makala hizi hapahapa Dar24, zinazomulika timu zote hadi yatakapoanza mashindano nchini Urusi. Pia, fuatilia YouTube channel ya Dar24 Media, kupata dondoo za historia ya fainali hizi, kupitia kipindi cha Zaidi na vipindi vingine.

Nikukumbushe tu kuwa kesho tutaanza kulimulika kundi B, lenye timu za taifa za Ureno, Hispania, Morocco, na Iran. Mwambie na rafiki.

Mwanafunzi afariki dunia jijini Mwanza
Video: Makonda ayakana Makontena Bandarini, CCM inajiua