Urusi imepanga upya uongozi wa operesheni zake za kivita nchini Ukraine, na kumteua Jenerali mpya mwenye uzoefu wa mapambano ya kivita ya Syria kusimamia vita vya Ukraine.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Afisa wa Kijeshi wa Urusi amber hakutaks kutajwa jina lake amesema kuwa kamanda wa wilaya ya kijeshi ya kusini mwa Urusi, Jenerali Alexander Dvornikov, sasa ndiye anayeoongoza vita ya Urusi dhidi ya Ukraine.

“Kamanda huyo ana uzoefu mkubwa wa operesheni za Urusi nchini Syria. Kwahiyo tunatarajia uongozi na udhibiti utaboreka,” Uteuzi mpya ulifanyika katika jaribio la kuimarisha uratibu baina ya vikosi mbalimbali, kwani makundi ya Urusi yamekuwa yakipangwa na kuongozwa na wakuu tofauti, alisema afisa. 

Urusi hadi sasa inahangaika kufikia malengo yake ya kivita, ikishindwa kuichukua miji muhimu kama vile Kyiv kabla ya hatimaye kuelekeza macho yake katika jimbo la Donbas mashariki.

Afisa huyo alisema kuwa mbinu za Urusi zimekuwa zikiwafanya warudishwe nyuma na vikosi vyenye askari wachache wa Ukraine wanaopigana kwa akili zaidi na kwa kushitukiza-licha ya Urusi kufikiriwa kuwania kikosi “kikubwa” chenye bataliani 100 zenye wanajeshi wenye ujuzi.

Hata hivyo avisa huyo amebaishisha kuwa bila kubadili mbinu zake, ni vigumu sana kwa Urusi kufanikiwa kwa malengo yao waliyojiwekea wenyewe.

Mwimbaji wa wimbo wa 'Ekwueme' afariki dunia
Odemba:Polisi Itoe amri Kajala arudi kwa Harmonize