Wabunge wa Umoja wa Ulaya, wanatarajiwa kuipa Urusi hadhi ya taifa linalodhamini ugaidi kutokana na matendo ya nchi hiyo katika vita vyake dhidi ya Ukraine.

Endapo hatua hiyo itafanikiwa, itakuwa mara ya kwanza kwa Umoja wa Ulaya kwa ujumla wake kufikia azma kama hiyo, lakini haijulikani itakuwa na maana gani.

Rais wa Urusi, Vladmir Puttin. Picha ya Foreign Policy.

Aidha, waraka ulioandaliwa na idara ya utafiti ya Bunge la Ulaya, umesema Urusi inayaelekeza mashambulizi yake kwa kuwalenga raia na miundombinu, ikiwemo hospitali, shule na vituo vya afya.

Hata hivyo, ikiwa Bunge la Ulaya litapitisha azimio hilo litakuwa ishara ya kulaani matendo ya Urusi nchini Ukraine na nje ya nchi hiyo.

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky. Picha ya Agenzia Nova.

Hadi sasa Marekani inajizuia kuichukulia Urusi hatua kama hiyo, kwa hoja ya kuzuia athari zisizokusudiwa katika mfumo wake wa sheria.

Matengenezo, Ukame chanzo upungufu wa umeme: TANESCO
Marais wakutana kusaka amani ya DRC