Rais wa Ukraine, Vlodymyr Zelensky amethibitisha ripoti ya mashambulizi ya makombora nchini humo hii leo Alhamisi, Februari 24.

Zelensky amesema kuwa Urusi imefanya mashambulizi ya makombora kwenye miundombinu ya Ukraine na walinzi wa mpakani.

Afisa mkuu wa serikali ya Ukraine pia amethibitisha ripoti hizo akisema mashambulizi ya makombora yalizinduliwa leo asubuhi huko Kyiv, pamoja na harakati za askari huko Odessa kusini mwa nchi hiyo.

Wanajeshi wa Urusi pia wamekuwa wakivuka mpaka wa Kharkiv, takriban maili 25 kutoka mpaka wa Urusi, yombo vya habari vya Ukraine pia vinaripoti kuwa baadhi ya vituo vya silaha ya kijeshi ya Ukraine na makao makuu ya kijeshi huko Kyiv yameshambuliwa.

Hali hii inatokea Baada ya Rais Vladimir Putin wa Urusi kutangaza “operesheni ya kijeshi” katika eneo la Donbas mashariki mwa Ukraine. Putin alisema Urusi ilikuwa ikijilinda kutokana na mashumbilio ambayo wamekuwa wakiyapata.

Aliwataka wanajeshi wa Ukraine kuweka chini silaha zao na kuacha uingiliaji wowote wa mataifa ya nje dhidi ya Urusi kutapata jibu la “papo hapo”, alisema

Misafara ya wanajeshi na vifaru imeingia Ukraine kutoka pande zote. Msafara mmoja umevuka kutoka Belarus kuelekea kaskazini mwa mji mkuu wa Kyiv. Mwingine umeingia kutoka Crimea kusini, ambayo Urusi ilitwaa kutoka Ukraine mnamo 2014

Urusi ilivyoingia Ukraine
Wavujisha siri za miamala ya wateja kukiona