Urusi imeitaka Marekani kuepuka kutumia hatua za kijeshi kujibu tuhuma za Syria kutumia makombora ya kikemikali dhidi ya raia na waasi.
Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa, Vasily Nebenzia jana aliionya Marekani kuwa italipa kwa hatua zozote za kuvunja sheria za kijeshi kama itaiadhibu Syria kwa njia hizo.
“Ninapenda tena kutoa wito kwenu kuachana na mpango mnaoendelea kuusuka wa kuishambulia Syria,” Vasily Nebenzia alisema.
Hata hivyo, viongozi wa nchi nyingi za Magharibi wamekubaliana kuwa watafanya kazi pamoja kuwalenga wale wote waliohusika na mashambulizi ya kemikali eneo la Douma nchini Syria.
Urusi na Iran ni washirika wakuu wa Serikali ya Syria inayoongozwa na Bashar Al-Assad, serikali ambayo Marekani na washirika wake wanaipinga.