Urusi imewafukuza wanadiplomasia 60 wa Marekani, na kufunga ubalozi uliopo St. Petersburg ikiwa ni majibu kwa kitendo cha Marekani kuwafukuza wanadiplomasia wa Urusi juu ya shutuma ya Uingereza kuhusu kuhusika kwa Urusi katika shambulio la jasusi wa zamani wa Urusi Sergei Kripal na binti yake huko Uingereza.
Hatua hiyo imetangazwa na waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Lavrov amesema kuwa nchi nyingine zilizowafukuza Warusi wasubiri majibu kwa vitendo kwani kila kitu kinafuata utaratibu.
”Urusi imeamua kujitenga Zaidi yenyewe, tunaangalia maamuzi ya kuchukua,” amesema Heather Nauert alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Hata hivyo, zaidi ya nchi ishirini zimewafukuza wanadiplomasia wa Urusi nchini mwao katika kuiunga mkono Uingereza.