Naibu wa kwanza wa balozi na mwakilishi wa kudumu wa Urusi Dmitry Polyanskiy amekanusha taarifa kuwa Urusi ilihusika kwenye shambulizi la kulipua hospitali ya watoto, katika mji wa Mariupol nchini Ukraine siku ya Jumatano Machi 9.

Polyanskiy amesema katika ujumbe wake kwenye mtandao wa Twitter kuwa eneo hilo la hospitali lilikuwa limetekwa na askari wake kabla ya shabulizi hilo.

“Urusi ilikuwa imetoa tahadhari katika taarifa iliyotoa siku mbili kabla, kwamba hospitali hiyo imegeuzwa eneo la kijeshi na Waukraine wenye misimamo mikali;, hivyo basi inasikitisha sana kuona Umoja wa Mataifa unasambaza taarifa hii isiyo na uthibitisho,” Polyanskiy alisema.

Mwakilishi huyo wa kudumu wa Urusi alikuwa akijibu ujumbe uliotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kufuatia shambulizi hilo la hospitali ya watoto, kwa kuilaani vikali Urusi kwa janga hilo.

“Shambulizi lilotekelezwa siku ya Jumatano kwenye hospitali ya watoto iliyoko katika mji wa Mariupol, Ukraine, mahali ambapo kuna wodi za akina mama na watoto, linatisha. Ukatili huu usio na maana unapaswa kukomeshwa.”

Mara tu baada ya maafisa wa serikali ya Ukraine kutangaza hapo jana kwamba ndege za kivita za Urusi zimeshambulia hospitali ya watoto, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenzsky aliituhumu Moscow kwa kutekeleza mauaji ya kimbari.

Sudan yajitenga na Dunia; Yaendelea kukuza uhusiano na Urusi
Morrison amtumia salamu Ibenge